Baada ya kufanya kikao cha dharura, utawala ghasibu wa Israel umewapa amri askari jeshi wake kuchukua hatua za kukabiliana vikali na wanamapambano wa Palestina na ikilazimu wafanye uvamizi mwingine wa kijeshi katika Ukanda wa Gaza kupitia operesheni za nchi kavu.
Amri hiyo imetolewa na utawala wa Kizayuni katika hali ambayo utawala huo ulifikia mapatano ya usitishaji mapigano na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kwa upatanishi wa serikali ya Misri.
Mmoja wa maafisa wa utawala huo ghasibu amedai kwamba wapiganaji wa Hamas wamekuwa wakirusha makombora katika maeneo ya walowezi wa Kiyahudi.
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo amesikika akisema kwamba utawala huo utatumia kila njia kuwaua wanamapambano wa Kiislamu wa Palestina ambao wamekuwa wakikandamizwa kwa miaka mingi na utawala huo unaokalia kwa mabavu ardhi zao.
Jumamosi iliyopita utawala huo wa kigaidi ulishambulia kwa ndege za kijeshi Ukanda wa Gaza na kuwaua shahidi wanachama 9 wa harakati ya Kiislamu ya Jihadul Islami na kwa njia hiyo kukiuka moja kwa moja mapatano ya usitishaji vita kati ya pande hizo.
Kufuatia uchokozi huo wa wazi harakati hiyo kufikia sasa imefyatua makombora 30 katika maeneo yanayodhibitiwa na utawala huo ambapo askari wake mmoja ameangamizwa na wengine wawili kijeruhiwa. 892343