Abdulfadhil amesema, mahujaji wa Misri waliokwenda kutekeleza ibada ya hija nchini Saudi Arabia wamekutana na mashaka mengi.
Ameongeza kuwa mahujaji wa Misri wamebanwa mno na kukutana na mashaka mengi hususan katika uwanja wa Arafa, Mina na Muzdalifa.
Amesema kuwa nafasi iliyotolewa na serikali ya Saudia kwa mahujaji wa Misri ilikuwa ndogo sana na kwamba tokea sasa msafara wa hija wa mahujaji wa nchi hiyo utasimamiwa na taasisi moja ili kuepusha matatizo yaliyojitokeza mwaka huu. 895475