IQNA

Kikao cha kuchunguza fikra za Imam Musa Sadr kufanyika Lebanon

21:53 - November 10, 2011
Habari ID: 2220142
Kikao ha 12 cha kuchunguza fikra za Imam Musa Sadr kimepangwa kufanyika tarehe 24 Novemba katika ukumbi wa UNESCO katika mji wa Beirut nchini Lebanon.
Kikao hicho kitafanyika kwa ushirikiano wa Taasisi ya Imam Sadr na Kituo cha Utafiti cha Imam Musa Sadr. Wanafikra na wasomi mbalimbali wamealikwa kuzungumza kwenye kikao hicho akiwemo Rubaba Sadr, dada yake Imam Musa Sadr na viongozi wa makundi mablimbali ya kidini, kisiasa na kijamii.
Mabadiliko katika fikra za kidini itakuwa maudhui ya kwanza itakayojadiliwa katika kikao hicho kitakachoanza saa nane alasiri kwa wakati wa Lebanon.
Ali Umlil, Balozi wa Morocco nchini Lebanon amealikwa kuzingumza katika kikao hicho ambapo amepanga kuzungumzia suala la changamoto zinazotokana na fikra finyu na misimamo ya kupindukia mipaka katika fikra za kidini.
Khalil Hamdan mwanachama wa Harakati ya Amal nchini Lebanon pia atazungumza katika kikao hicho kuhusiana na mchango wa shughuli za kijamii katika kuleta mabadiliko yanayotakiwa nchini. 895573
captcha