Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah amesema kuwa kama madola ya kibeberu yataishambulia Iran basi uchokozi wao huo utazusha vita vya kila upande katika eneo la Mashariki ya Kati.
Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo na kuongeza kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani zinataka kudhoofisha muqawama kwa kuzifanya Iran na Syria zifikirie kujihami binafsi wakati wote na kuachana na misimamo yao ya kuendeleza mupambano.
Aidha Sayyid Hassan Nasrullah amesema, Marekani inapaswa kufahamu kuwa, vita dhidi ya Iran na Syria havitoishia katika nchi hizo mbili pekee bali vitasambaa katika nchi nyinginezo za eneo hili.
Vilevile ameashiria matukio ya hivi sasa ya Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika, na kusema kuwa, mabadiliko ya tawala katika nchi za Tunisia, Libya na Misri yamekwenda kinyume na maslahi ya Marekani na Israel na kwamba hiyo ni moja ya sababu zinazopelekea madola hayo mawili ya kibeberu yatake kumalizia hasira zao kwa Iran na Syria.
896569