IQNA

Mwamko wa Kiislamu ni pigo kubwa kwa utawala wa Kizayuni

16:28 - November 16, 2011
Habari ID: 2223384
Utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umekuwa ukitenda jinai dhidi ya Waislamu kwa miongo kadhaa hivi sasa unakabiliwa na changamoto kubwa ambayo ni mwamko wa Kiislamu, amesema mbunge mmoja wa Iran.
Katika mahojiano yake na IQNA, Hujjatul Islam Malek Mohammadi ambaye ni mwanachama wa Kamati ya Utamaduni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa changamoto hiyo ambayo pia ni tishio kwa waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni ni bishara ya kufika ukingoni utawala huo ghasibu.
Ameongeza kuwa mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika una misingi yake katika fikra zenye muongozo wa busara za mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini na vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Khamenei.
Mbunge huyo wa Iran ameashiria nafasi ya vyombo vya habari katika kuimarisha mwamko wa Kiislamu na kusema vyombo vya habari vimekuwa na nafasi nzuri katika kusambaza habari za mafanikio ya mapinduzi ya Kiislamu pamoja na kufichua njama za maadui na kusisitiza kuhusu umuhimu wa umoja na mshikamano wa Waislamu duniani.
Hujjatul Islam Malek Mohammadi ameashiria harakati ya ‘Kuikalia Wall Stree’ huko Marekani na kusema harakati dhidi ya mfumo wa kibepari itaendelea. Ameongeza kuwa madola makubwa ya kishetani kama vile Marekani na Uingereza hayako katika nafasi ya kusimama dhidi ya azma ya mataifa. 899237
captcha