Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kiwanda cha uchapishaji cha Iqra na mwanahabari wa Nigeria Badmos Aliyou Albi katika mahojiano yake na shirika la habari la IQNA. Amesema wananchi wanamapinduzi wa kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati wanataka kujiamulia mambo yao wenyewe na kuchagua serikali zitakazoongoza nchi kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Amesema serikali katika nchi za kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati zilikuwa zikiongozwa na vibaraka wa nchi za Magharibi na kujali zaidi maslahi ya Wamagharibi. Amesisitiza kuwa baada ya kuondolewa madarakani serikali hizo vibaraka, sasa wananchi watachukua maamuzi yote kuhusu maslahi na jinsi ya kuendesha nchi zao.
Amewatahadharisha wananchi katika nchi zilizofanya mapinduzi juu ya kuingia madarakani watu au makundi vibaraka ambayo yumkini yakarejesha tena serikali zinazofanana na zile zilizong'olewa madarakani. Amesema wananchi wanapaswa kuwa macho na kulinda matunda ya mapinduzi yao. 902888