IQNA

Vijana Waislamu walitumia intaneti katika mwamko wa Kiislamu

16:38 - November 23, 2011
Habari ID: 2227216
Tokea siku za awali za mwamko wa Kiislamu katika nchi za Kiarabu, vijana katika nchi hizo walitumia mitandano ya intaneti kueneza habari na ripoti za mwamko.
Haya ni kwa mujibu wa Rasha Ashahid Ali, mwanaharakati wa vyombo vya habari kutoka Misri ambaye pia ni mtaalamu wa intaneti na tovuti za habari za kijamii.
Akizungumza na IQNA, amesema kuna vyombo vya habari vya aina mbili, vinavyoeneza hitilafu na chuki katika mataifa na vinavyoripoti matukio bila kupendelea.
‘Vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kuzidisha au kupunguza migongano’, amesisitiza. Bi. Rasha Ashahid Ali. Ameelezea masikitko yake kuwa baadhi ya mitandandao ya intaneti inajishughulisha na kueneza chuki za kidini baina ya Waislamu. Amesema vyombo vya habari vya Kiislamu vinapaswa kutumika kupambana na fikra potofu.
897073
captcha