IQNA

Utawala wa Kizayuni wafanya njama za kuzuia adhana Palestina

10:02 - December 11, 2011
Habari ID: 2236382
Utawala wa Kizayuni wa Israel utaanza kuchunguza rasimu ya sheria ya kupiga marufuku adhana katika ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu na Wazayuni mwaka 1948.
Rasimu hiyo ambayo itaanza kuchunguzwa leo ni sehemu ya mipango ya utawala ghasibu wa Israel ya kufuta kabisa athari za Kiislamu huko Palestina.
Rasimu ya sheria hiyo iliwasilishwa na chama cha Yisrael Beiteinu cha Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala huo ghasibu Avigdor Lieberman katika Bunge la Israel miezi kadhaa iliyopita lakini bunge hilo halikuipasisha kutokana na unyeti unaohusu kadhia yenye. Chama hicho sasa kimefanikiwa kumshawishi Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanhayu kuhusu rasimu hiyo ya sheria ya kibaguzi.
Spika wa Bunge la Israel amesema kuwa kupasishwa rasimu hiyo ni sawa na kutangaza vita dhidi ya Waislamu na utekelezaji wake unahitaji kuwepo idadi kubwa ya askari polisi katika maeneo ya mijini na vijijini, jambo ambalo amesisitiza kuwa litazusha mapigano kati ya raia na polisi. 912614


captcha