Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Ban Ki-moon ameutaka utawala haramu wa Israel kusitisha mara moja ujenzi wa vitongoji hivyo katika mji wa Beit Lahm. Amesema ujenzi wa vitongoji hivyo unakiuka sheria za kimataifa.
Nayo Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ilitoa taarifa hapo siku ya Jumamosi ikilaani vikali uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kujenga vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika eneo la Ras al-Amud katika kata ya kati huko Quds Tukufu.
Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC amesema kwamba kuendelea miradi ya ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Wapalestina ni jambo linalokwenda kinyume na sheria za kimataifa pamoja na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
914926