IQNA

Kikao cha kimataifa cha Nafasi ya Kisiasa ya Wanawake wa Kiislamu chaanza Uturuki

17:07 - December 21, 2011
Habari ID: 2242699
Kikao cha kimataifa cha Nafasi ya Kisiasa ya Wanawake katika Ulimwengu wa Kiislamu kimeanza leo Jumatano katika mji wa Istanbul nchini Uturuki.
Kwa mujibu wa Tovuti ya ABC. AZ kikao hicho kinafanyika kwa udhamini wa Jumuiya ya Kibunge ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Wizara ya Familia na Siasa za Kijamii ya Uturuki. Rajab Tayyib Erdogan, Waziri Mkuu wa Uturuki ndiye aliyefungua kongamano hilo.
Kongamano hilo litachunguza na kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na nafasi ya mwanamke katika ulimwengu wa Kiislamu, yakiwemo ya usawa kati ya mwanamke na mwanaume, kushirikishwa mwanamke katika uimarishaji wa siasa na demokrasia, haki za wanawake katika mabadiliko ya kisiasa ya Mashiriki ya Kati ka na kaskazini mwa Afrika, Uislamu na demokrasia na kuzinduliwa mashirika na taasisi zitakazopigania usawa na uadilifu wa kijinsia katika jamii.
Kongamano hilo limepangwa kuendelea hadi tarehe 25 Disemba. 919487
captcha