IQNA

Mwanamfalme wa Saudia kuanzisha televisheni ya uchochezi dhidi ya mapinduzi ya kieneo

17:14 - December 29, 2011
Habari ID: 2247519
Mwanamfalme tajiri wa Saudia ana mpango wa kuanzisha televisheni ya satalaiti nchini Bahrain kwa jina la al-Arab, kwa madhumuni ya kuvuruga mapinduzi ya kieneo, kueneza siasa za Aal Saud na pia uchochezi dhidi ya Iran.
Kwa mujibu wa CNN Mwanamfalme Walid bin Talal ana mpango wa kuanzisha televisheni hiyo itakayoendesha shughuli zake chini ya shirika la habari la Rotana na katika mkondo uleule wa siasa za televisheni nyingine za Kiarabu za Al-Jazeera na al-Arabiya kwa kisingizio cha kusaidia kuimarisha uchumi wa Bahrain ambao anadai umeathirika vibaya kutokana na harakati za mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo.
Talal amesema kwamba televisheni hiyo ambayo amedai kuwa ni uhuru itakuwa ikipeperusha hewani vipindi vyake kwa lengo la kuimarisha hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Saudi Arabia na ulimwengu wa Kiarabu.
Kwa kudai kuwa televisheni hiyo itashindana na televisheni nyingine za Kiarabu za al-Jazeera na al-Arabiyya ni wazi kuwa televisheni zote hizo tatu zitashindana kuchochea hisia dhidi ya mapinduzi ya wananchi katika Mashariki ya Kati, madhehebu ya Shia na kuunga mkono siasa za ukoloni na ubeberu wa nchi za Magharibi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Viongozi wa Bahrain tayari wameunga mkono kuanzishwa nchini humo televisheni hiyo. Televisheni ya al-Arab itaanzishwa na kuendeshwa nchini Bahrain kwa ushirikiano wa shirika la Marekani la Bloomberg LP. 924890
captcha