IQNA

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu yalaani ujenzi wa nyumba 130 za Wazayuni

10:22 - January 02, 2012
Habari ID: 2249546
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC amelaani vikali uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kutaka kujenga nyumba mpya 130 za Wazayuni huko Quds na hasa mashariki mwa eneo hilo takatifu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Kuwait KUNA, Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC ametoa taarifa kuhusiana na suala hilo akisema kuwa siasa za kichokozi zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina zinakiuka maazimio na sheria za kimataifa.
Ihsanoglu amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Kamati ya Pande Nne ya Amani kuchukua hatua za haraka ili kuzuia na kusimamisha mara moja hujuma za mara kwa mara zinazotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
Licha ya uchokozi, uchochezi na uvunjaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina, hivi karibuni utawala huo ulitangaza kwamba Quds Tukufu ni mji mkuu wake, jambo ambalo limepingwa vikali na mataifa mengi ya dunia na kutambuliwa kuwa halina itibari yoyote ya kisheria. 926906
captcha