Katika kipindi hicho cha siku 10 ratiba mbalimbali za maombolezo ya Arbaini ya Imam Hussein (as), makumbusho ya kifo cha Mtume (saw) na kuuawa shahidi Maimamu Hassan Mutaba na Imam Ali bin Musa ar-Ridha (as) zitatekelezwa.
Kwa mnasaba huohuo, maombolezo mengine kama hayo ya siku 10 yamepangwa kufanyika katika Kituo cha Kiislamu cha London kuanzia tarehe 14 Januari ambayo inasadifiana na Arbaini ya Imam Hussein (as).
Wanazuoni na wanafikra wa Kiislamu wamepangiwa kuzungumza katika maombolezo hayo kuhusiana na pande mbalimbali za maisha na kujitolea kwa watukufu hao katika kulinda dini tukufu ya Kiislamu. 931628