IQNA

Kulindwa Syria kunadhamini usalama wa nchi za Kiarabu na Kiislamu

17:04 - January 17, 2012
Habari ID: 2258301
Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Mashia wa Lebanon amesisitiza kwamba Waislamu wanapasa kufanya juhudi za kulinda usalama na umani ya Syria kwa sababu jambo hilo linalinda usalama na uthabiti wa nchi zote za Kiarabu na Kiislamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya nowlebanon, hayo yamesemwa na Ayatullah Abdul Amir Qabalan, Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Mashia wa Lebanon alipokutana na kuzungumza na Ahmad Davutoglu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki aliyekuwa safarini nchini Lebanon hivi karibuni.
Ayatullah Qabalan amesema Walebanon wanapinga vikali kila aina ya fitina za kimadhehebu na kikabila na kuunga mkono umoja wa kitaifa na Kiislamu. Ameendelea kusema kwamba Waislamu wote wanapasa kushirikiana na kuimarisha umoja wao katika kupambana na utawala haramu wa Israel ambao ameutaja kuwa shari mutlaki katika eneo la Mashariki ya Kati na ambao ni chimbuko la matatizo na fitina zote katika eneo hilo.
Amesema utawala huo umekuwa ukitekeleza njama nyingi hatari dhidi ya mataifa ya Kiarabu na Kiislamu katika Mashariki ya Kati.
Kuhusiana na suala la Syria Ayatullah Qabalan amesema kuwa kuna haja ya kushirikiana Uturuki na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kulinda umoja wa kitaifa wa Syria kwa sababu nchi hiyo iko katika mstari wa mbele wa kupinga ugaidi, kupambana na taasubi na kila aina ya fitina za kimadhehebu.
Amesema Syria iko katika safu ya kwanza ya kupambana na utawala haramu wa Israel pamoja na jinai zake na kwa hivyo kuna udharura mkubwa wa kulindwa uthabiti wa nchi hiyo. 936206
captcha