IQNA

Kongamano la ‘Wanawake Waislamu katika Mabunge ya Nchi za Kiislamu’ lamalizika

8:59 - January 29, 2012
Habari ID: 2263720
Kongamano la ‘Wanawake Waislamu katika Mabunge ya Nchi za Kiislamu’ lilimalizika Ijumaa 27 Januari katika mji wa Plumpang katika mkoa wa Sumatra Kusini nchini Indonesia.
Kwa mujibuwa mwandishi wa IANQ, kongamano hilo la siku moja limefanyika katika fremu ya kuendeleza mkutano wa Jumuiya ya Mabunge ya Nchi za Kiislamu ulioanza tarehe 24 Januari nchini Indonesia.
Mkutano huo ulijadili nafasi ya wanawake katika ustawi na uimarishwaji demokrasia katika nchi za Kiislamu, nafasi ya jumuiya za kijamii za Kiislamu, haki za wanawake Waislamu na uwezo wa wanawake Waislamu katika kutatua matatizo na kupunguza masaibu ya wanawake na watoto Waislamu huko Palestina.
Jumuiya ya Mabunge ya Nchi za Kiislamu inajumuisha mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na ilianzishwa mwaka 1999 mjini Tehran katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
941776
captcha