IQNA

Toleo jipya la Jarida lililomvunjia heshima Mtume (saw) lapigwa marufuku Morocco

13:28 - January 31, 2012
Habari ID: 2265516
Serikali ya Morocco imepiga marufuku usambazaji na uuzaji wa toleo la hivi karibuni la jarida la Ghazal, ambalo limemvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Kwa mujibu wa tovuti ya atlasinfo, serikali ya Morocco imechukua hatua ya kusimamisha toleo la hivi karibuni la jarida hilo linalochapishwa kwa lugha ya Kifaransa kutokana na kuchapisha picha zinazomvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw).
Wizara ya Habari ya Morocco imesema kuwa serikali imechukua hatua hiyo kutokana na ukweli kwamba picha hizo ni aina ya dharau kwa Mtume na Waislamu. Taarifa ya Wizara hiyo imesema inasikitisha kuona kwamba baadhi ya magazeti na majarida ya kigeni yamepuuza maazimio ya Baraza Kuu la Umoja ya Mataifa yanayosisitiza umuhimu wa kupambana na mielekeo ya kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini na kuvitaka vyombo vya habari kujiepusha kudharau wafuasi wa dini tofauti, jambo ambalo limepelekea serikali ya Morocco kuyachukulia hatua za kisheria mashirika na jumuiya zinazokiuka maazimio hayo.
Ni vyema kukumbusha hapa kwamba mwezi uliopita pia serikali ya Morocco ilipiga marufuku uuzwaji wa jarida jingine la Kifaransa kwa jina la Express kutokana na kumvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw). Gazeti hilo lilichapisha picha za kumbeza Mtume (saw) kutoka gazeti jingine la Kifaransa kwa lengo la kuzisambaza katika nchi za Kiarabu. 944091
captcha