IQNA

Makaburi ya kwanza rasmi ya Waislamu yazinduliwa Ufaransa

12:05 - February 07, 2012
Habari ID: 2269989
Makaburi ya kwanza rasmi ya Waislamu yamezinduliwa katika mji wa Strasbourg mashariki mwa Ufaransa.
Shughuli ya kuzindia makaburi hayo iliyofanyika Jumatatu tarehe 6 Februari imehudhuriwa na Naibu Meya wa Strasbourg Anne-Pernelle Richardot ambaye amesema, 'sheria za eneo la Alsace-Moselle zinaturuhusu kutenga makaburi yatakayosimamiwa na baraza la mji'. Ameongeza kuwa katika miji mingine ya Ufaransa eneo maalumu hutengwa kwa ajili ya Waislamu katika makaburi ya umma.
Ardhi ya makaburi ya Waislamu Strasbourg imegharimu Euro 800,000 ambapo pia hapo kuna eneo la kuoshea na kuswalia maiti.
Waislamu nchini Ufaransa wanasema haitoshi kutengewa eneo katika makaburi ya umma na wanataka kila eneo liwe na makaburi maalumu ya Waislamu. Baraza la Masuala ya Waislamu Ufaransa limesema ni haki ya kisheria kwa Waislamu kupewa makaburi yao maalumu kwani wao pia wana mizizi na asili Ufaransa.

948253
captcha