Kwa kushambulia maeneo yao wenyewe, Wazayuni wanaoishi Marekani wana lengo la kuonyesha kuwa mashambulio hayo yanafanywa na Waislamu na hivyo kuchochea chuki dhidi ya Waislamu hao na dini tukufu ya Kiislamu.
Kuhusiana na suala hilo, David Haddad Myahudi mwenye umri wa miaka 56 anayefungamana na lobi ya Wazayuni wa Marekani ambaye wiki iliyopita alitiwa nguvuni na askari usalama wa Marekani amekiri kwamba amekuwa akishirikiana na makundi kadhaa ya Mayahudi walio na misimamo ya kupindukia mipaka na waungaji mkono wa utawala haramu wa Israel kwa lengo la kushambulia vituo na maeneo ya Mayahudi nchini Marekani na kuandika nara zilizo dhidi ya Mayahudi katika maeneo hayo na kisha kudai kuwa vitendo hivyo vinafanywa na Waislamu.
Amesema wamekuwa wakifanya vitendo kama hivyo vya kichochezi dhidi ya Waislamu kwa lengo la kuuokoa utawala haramu wa Israel.
David Haddad amedai kwamba wanatambua vyema kuwa Marekani haiwezi kuwa na nafasi yoyote muhimu katika kuwarejesha Mayahudi katika ardhi alizodai kuwa waliahidiwa kwa hivyo ni jukumu lao kuwatanabaisha Mayahudi na kuwasihi warejee katika ardhi hizo. 949057