IQNA

Kiongozi wa Mashia wa Thailand asema Mosad na Mujahidina Khalq ndio waliohusika na milipuko ya kigaidi

16:04 - February 22, 2012
Habari ID: 2278714
Sayyid Suleiman Husseini, Kiongozi wa Mashia wa Thailand amesema mbele ya vyombo vya habari vya nchi hiyo kwamba milipuko ya kigaidi ya hivi karibuni huko Bangkok, mji mkuu wa nchi hiyo ilitekelezwa kwa ushirikiano wa karibu wa shirika la kijasusi la utawala haramu wa Israel Mossad na kundi la magaidi wa Mujahedina Khalq.
Kwa mujibu wa tovuti ya mondialisation, Sayyid Suleiman amesema kuwa ugaidi huo umetekelezwa na makundi hayo kwa lengo la kuchafua jina la Jamhuri ya Kiislamu duniani.
Amesema makundi mawili hayo ya kigaidi yameshirikiana kutekeleza milipuko hiyo ili kuonyesha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inahusika na vitendo vya ugaidi duniani. Amesema yametekeleza ugaidi huo ili kuishinikiza Iran ilegeze msimamo na kusalimu amri mble ya matakwa yao haramu na ya vibaraka wao wa Magharibi.
Sayyid Suleiman ameongeza kuwa Wairani wote wanaotuhumiwa kuhusika na milipuko hiyo ni wanachama wa kundi la Mujahidina khalq lililo na kambi yake ya kijeshi nchini Iraq na ofisi ya kisiasa mjini Paris Ufaransa. 958166
captcha