Sheikh Kazem Sidiqi amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa na kubainisha kwamba, ushiriki mkubwa wa wananchi katika uchaguzi wa Bunge uliofanyika leo ni pigo kubwa kwa maadui wa taifa hili. Khatibu wa Sala ya Ijumaa ameashiria pia njama za maadui dhidi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu unaotawala hapa nchini na kusema kwamba, kama ilivyokuwa huko nyuma wananchi wa Iran wataleta hamasa nyingine kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi na kumkatisha tamaa adui. Amesema, propaganda kubwa za maadui ni ishara ya woga na wasi wasi mkubwa walionao maadui kwa taathitra ya Mapinduzi ya Kiislamu katika eneo hili. Sheikh Kazem Sidiqi ameashiria kitendo cha kishenzi cha hivi karibvuni cha wanajeshi wa Marekani cha kuivunjia heshima Qur'ani tukufu kwa kuichoma moto huko Afghanistan na kusema, kitendo hicho cha wananjeshi wa Marekani ni kuwatusi na kuwanjia heshima wanadamu na vitabu vingine vya mbinguni.
963716