Sambamba na kuashiria ushiriki wa asilimia 64 wa wananchi katika uchaguzi wa Bunge la 9 la Iran wiki iliyopita, Ayatullah Ahmad Jannati amesema, katika uchaguzi huo kutokana na kuwa macho na kwa umaizi waliokuwa nao, Wairani walivuruga njama na mipango yote ya maadui ya kuudhuru Mfumo na Mapinduzi ya Kiislamu.
Aidha huku akisisitiza kuwa uchaguzi wa Bunge la Iran ulifanyika kwa uhuru kamili na kwa hamasa kubwa nchini kote, Ayatullah Jannati ameongeza kuwa, kwa kushiriki kwa wingi kwenye uchaguzi huo wananchi wa Iran wameonyesha uwezo na izza waliyonayo dhidi ya maadui hasa Marekani na washirika wake.
Katika upande mwingine Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amelaani jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Khalifa na Aal Saudi nchini Bahrain na kusema kwamba, jinai hizo zinatekelezwa kwa uungaji mkono wa pande zote wa Washington huku jamii ya kimataifa ikizinyamazia kimya.
968290