IQNA

Iran yalaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina huko Gaza

13:53 - March 12, 2012
Habari ID: 2290314
Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetangaza kuwa mashambulio ya hivi karibuni ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Gaza wasio na ulinzi huko Palestina na ambayo hadi sasa yameshauwa shahidi Wapalestina 18, ni jinai za kivita.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeeleza kuwa, kuuawa kigaidi Zohair al Qaisi Katibu Mkuu wa Kamati za Mapambano ya Wananchi wa Palestina (PRC) na wenzake kadhaa ni katika jinai za ugaidi wa kiserikali unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeongeza kuwa, inashangaza kuona jamii ya kimataifa na wale wanaodai kutetea haki za binadamu wakiendelea kukaa kimya bila ya kuchukua hatua yoyote. Taarifa hiyo imesisitiza pia kwamba, taasisi za kimataifa na zile za kutetea haki za binadamu zinapaswa kutekeleza majukumu yao ya kibinadamu na kisheria mbele ya ukiukaji wa haki za binadamu na pia kuuawa shahidi raia wa Palestina wasio na hatia kunakofanywa na utawala haramu wa Kizayuni.
969994
captcha