IQNA

Malaysia kuwa nchi ya kwanza ya Kiislamu iliyostawi kikamilifu

11:38 - April 08, 2012
Habari ID: 2299935
Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Tun Abdulrazak ametoa wito kwa taasisi za Kiislamu nchini humo kuisaidia Malaysia kuwa nchi ya kwanza ya Kiislamu iliyofikia kiwango cha nchi iliyostawi kikamilifu.
Akizungumza Aprili 7 mjini Putrajaya, Abdulrazak ameelezea matumaini kuwa kutokana na hima ya taasisi hizo za Kiislamu ndoto ya Malaysia kuwa nchi iliyostawi itafikiwa.
'Nina ndoto. Nataka Malaysia iwe nchi ya Kiislamu, tufanyeni historia kwa kuwa nchi ya kwanza ya Kiislamu kufikia kiwango cha ustawi kamili,' amesema katika hafla ya jumuiya za Kiislamu nchini Malayasia. Amesema Malaysia ikifikia daraja ya nchi iliyostawi kikamilifu serikali itaweza kufadhili zaidi taasisi za Kiislamu na hivyo kuinua hadhi ya Uislamu.
Wanachama 5,000 wa taasisi za Kiislamu walihudhuria hafla hiyo ambapo Waziri Mkuu Abdulrazak amewapongeza kwa ushiriki wao katika ajenda ya maendeleo.
Waziri Mkuu wa Malaysia alitangaza bajeti ya serikali yenye lengo la kuimarisha shughuli za misikiti na madrasa ambapo ameyataja maeneo hayo mawili ya kidini kuwa ni 'moyo ya jamii.
980647
captcha