IQNA

Iran yasisitiza haki yake ya kunufaika na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani

15:38 - April 08, 2012
Habari ID: 2300099
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu haki ya Iran ya kunufaika na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani.
Ali Akbar Salehi ameyasema hayo mjini Tehran alipokutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa zamani wa Japan Yukio Hatoyama. Salehi amesema Iran kama mwanachama wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki na Mkataba wa Kuzuia Utengenezaji na Usambazaji Silaha za Atomiki NPT, ina haki ya kuendeleza shughuli zake za nyuklia kwa malengo ya amani. Amesema Iran inataka amani, utulivu na usalama katika eneo la Mashariki ya Kati na dunia nzima. Salehi ameongeza kuwa utamaduni wa Iran umejengeka katika misingi ya amani, urafiki na kuimarisha uhusiano na nchi zingine duniani.
Kwa upande wake Yukio Hatoyama ambaye pia ni mbunge mwandamizi katika bunge la Japan amesema kikao kijacho cha Iran na kundi la 5+1 kina umuhimu mkubwa. Ameelezea matumaini yake kuwa kadhia ya nyuklia ya Iran itatatuliwa kwa amani kwani utumiaji wa teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani ni haki ya nchi zote.
980577
captcha