Ameyasema hayo katika mkutano wake na Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Bangkok Mostafa Najjarianzadeh.
Sheikh Ismail amesisitiza kuwa Waislamu nchini Thailand wanaitazama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama nchi yenye nguvu isiyojidhalilisha mbele ya madola ya kibeberu.
Kwa upande wake Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Bangkok amempongeza Sheikh Ismail kwa juhudi zake za kuimarisha hali ya Waislamu nchini humo.
Amesema Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Bangkok kiko tayari kuimarisha ushirikiano na taasisi za Kiislamu nchini Thailand.
Wawili hao walijadili njia za kuimarisha harakati za Kituo cha Utamaduni cha Iran na kuarifisha Iran kwa Waislamu wa Thailand.
984906