Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia maandamano yaliyofanywa na vyama na makundi mbalimbali ya Mauritania dhidi ya kitendo kiovu cha kiongozi wa jumuiya hiyo.
Al Abidi alitiwa nguvu wakati alipokuwa akishauriana na wanachama wa chama hicho juu ya matukio hayo mjini Nouakchott.
Ijumaa iliyopita kiongozi huyo wa Jumuiya ya Mapambano kwa Ajili ya Ukombozi alitoa amri ya kuchomwa moto vitabu kadhaa vya Kiislamu kwa kisingizio kwamba waandishi wa vitabu hivyo wanahalalisha utumwa nchini Mauritania. 995904