Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR), Jumamosi, lilikemea mauaji ya angalau watu sita, akiwemo mwanamke, katika harusi Gaza, likiutaja kama ukiukaji mwingine wa “usitishaji mapigano”. CAIR pia imemtaka Rais wa Marekani Donald Trump na wakuu wa mataifa yenye Waislamu wengi kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel uheshimu mapatano ya usitishaji vita.
Ripoti moja ilionyesha kuwa utawala wa Kizayuni pia ulimuua mtoto mchanga katika shambulio hilo.
Tangu kutangazwa kwa “usitishaji mapigano”, Israel imeua karibu Wapalestina 400. Aidha tangu Oktoba 2023, majeshi ya Israel yameua zaidi ya watu 70,000 Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Inaaminika idadi halisi ya vifo ni kubwa zaidi.
Katika tamko lake, CAIR lilisema: “Kushambulia sherehe ya harusi ni tendo la ukatili linaloonyesha wazi kutokuwa na maana kwa kile kinachoitwa ‘usitishaji mapigano’. Mauaji ya makusudi ya raia yanasisitiza haja ya dharura kwa Rais Trump na mataifa ya Kiarabu ya Kiislamu yaliyodhamini mapatano ya usitishaji huo kuchukua hatua. Hakuna usitishaji wa kweli wa mapigano wakati utawala wa Kizayuni unaendelea kuua watu Gaza bila kuadhibiwa. Serikali yetu na jumuiya ya kimataifa lazima zikomeshe kuhalalisha ukatili huu na kudai mwisho wa mashambulizi yote, pamoja na uwajibikaji kwa uhalifu huu wa kivita.”
CAIR pia liliwataka Wamarekani wote kuwasiliana na Bunge la Marekani kudai serikali ya Israel ikomeshe mara moja kuzuia kuingia kwa mahema ya baridi na misaada ya kibinadamu Gaza, huku watoto wakipoteza maisha kwa baridi kali kutokana na vizuizi vya Israel.
3495805