Mashindano haya yamepewa jina la “Tuzo ya Mfalme Salman bin Abdulaziz” na yameandaliwa na Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Da‘wa na Mwongozo.
Lengo lake ni kuendeleza shughuli za Qur’ani Tukufu nchini humo katika ngazi mbalimbali.
Awamu ya mwanzo inafanyika katika makundi sita, yakiwa yamegawanywa kwa wasichana na wavulana katika maeneo tofauti ya Saudi Arabia, kama maandalizi ya hatua ya mwisho.
Fainali zitafanyika katika mwezi wa Sha‘ban kwa kalenda ya Hijri, mjini Riyadh, ambapo washindi bora watawasilishwa.
Kwa mujibu wa waandaaji, jumla ya riyal milioni 7 za Kisaudi zimetengwa kwa mashindano haya, na zawadi hizi zitawapewa washindi wa juu katika makundi sita.
Sherehe ya kuwaheshimu washindi wa upande wa wavulana itafanyika tarehe 20 Februari 2026 mjini Riyadh, na sherehe ya wasichana itafanyika siku inayofuata katika mji mkuu wa Saudi Arabia.
3495802