IQNA

Ripoti: Mufti wa zamani wa Syria ahukumiwa kifo

15:08 - December 11, 2025
Habari ID: 3481646
IQNA – Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa Sheikh Badreddin Hassoun, aliyewahi kuwa Mufti Mkuu wa Syria katika utawala wa Bashar al-Assad, amehukumiwa adhabu ya kifo.

Kwa mujibu wa Arabi 21, vyombo vya habari vya Syria vimechapisha taarifa zikidai kuwa hukumu ya kifo imetolewa dhidi ya mufti huyo wa zamani. Inaelezwa kuwa Hassoun, ambaye alikamatwa miezi kadhaa iliyopita, amehukumiwa kifo pamoja na baadhi ya maafisa wengine wa serikali iliyopita.

Hata hivyo, Mazhar Abdul Rahman al-Wais, waziri wa sheria katika serikali mpya ya Syria, amekanusha uvumi huo. Katika taarifa yake, alisema kuwa kesi ya Hassoun bado iko katika hatua za kimahakama na tayari imehamishwa kutoka wizara ya sheria kwenda kwa hakimu mpelelezi wa wizara ya mambo ya ndani.

Alisema: “Iwapo hakimu atabaini kuwa Hassoun ana hatia kwa mujibu wa sheria, atatoa hukumu na kuiwasilisha kwa mahakama husika; na akimkuta hana hatia, basi ataachiwa huru.”

Kufuatia kauli za mwana wa Sheikh Badreddine Hassoun kuhusu hali ya afya ya baba yake kudhoofika, al-Wais alikanusha madai hayo na kusema kuwa Hassoun yuko katika hali nzuri na anafuatiliwa kiafya akiwa gerezani.

Mwezi Agosti mwaka jana, wizara ya 'sheria' ya utawala wa sasa Syria ilitoa sehemu ya mahojiano ya uchunguzi dhidi ya watu mashuhuri wa serikali iliyopita, akiwemo Sheikh Badreddine Hassoun, Brigedia Jenerali Atef Najib (aliyekuwa mkuu wa kitengo cha usalama wa kisiasa), Mohammed al-Shaar (waziri wa mambo ya ndani wa zamani), na Meja Jenerali Ibrahim Hawija (aliyekuwa mkuu wa Idara ya Ujasusi wa Jeshi la Anga).

Hakimu mpelelezi alimshutumu bila msingi Sheikh Hassoun kwa makosa ya “uchochezi, ushiriki na kuhusika katika mauaji.”

3495698

Habari zinazohusiana
captcha