
Mpango huu, uliozinduliwa kwa ushirikiano na Idara ya Miskiti, unahusisha washiriki 50 walioteuliwa kupitia mchujo mkali, ili kuimarisha usomaji wa Qur’ani Tukufu kwa riwaya ya Ḥafs ‘an ‘Āṣim, kwa mnyororo wa upokezi usiokatika unaofika moja kwa moja kwa Mtume Muhammad (SAW). Hatua hii ni sehemu ya juhudi za wizara kuendeleza usomaji sahihi na wa kina wa Qur’ani kwa mujibu wa kanuni za tajwīd na qirā’āt zilizoidhinishwa na wanazuoni.
Usajili wa mpango huu ulifunguliwa Novemba 24, 2025 na kudumu kwa wiki moja, ambapo takribani maimam na makhatibu 600 kutoka maeneo mbalimbali ya Qatar walijisajili. Baadaye walifanyiwa mitihani katika Msikiti wa Hamad bin Nasser Al Misned, Hazm Al Markhiya, kati ya Desemba 7–11, 2025. Washiriki walipimwa kwa viwango vya kielimu vilivyothibitishwa, ikiwemo usahihi wa usomaji na uhifadhi wa Qur’ani. Hatimaye, maimam 50 bora walichaguliwa kushiriki katika mpango wa miezi sita, unaotarajiwa kukamilika Juni 11, 2026.
Ili kuhakikisha ubora wa mafunzo, Idara ya Da‘wah iliwateua walimu 10 wenye vyeti na utaalamu wa qirā’āt, waliotawanywa katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kurahisisha mahudhurio ya washiriki na kuongeza ufanisi wa mafunzo. Kuendelea kwa awamu hii kunathibitisha mafanikio ya mpango wa “Asaneed” katika kufanikisha malengo yake, huku Wizara ya Awqaf ikiendeleza uwekezaji katika vipaji vya binadamu na kuimarisha nafasi ya miskiti. Lengo kuu ni kuhakikisha Qur’ani Tukufu inasomwa kwa usahihi na kwa kiwango cha juu cha kielimu na kifundishaji katika maisha ya jamii ya Kiislamu.
3495827