
Jumapili alasiri, nakala ya Qur’an Tukufu ilipatikana ikiwa imefungwa kwa minyororo kwenye ngazi za kuingia msikitini, ikiwa na mashimo sita ya risasi na stika yenye ujumbe wa vitisho: “Asante kwa ziara, lakini sasa ni wakati wa kurudi nyumbani.” Ujumbe huo uliandikwa kwa Kiarabu na Kiswidi, ukionyesha wazi nia ya mhalifu. Tukio hili liliwashtua waumini na wakazi wa eneo hilo, hasa ikizingatiwa kuwa jamii hiyo imekuwa ikilengwa mara kwa mara na makundi ya mrengo wa kulia wenye chuki dhidi ya Uislamu.
Wawakilishi wa msikiti walilitaja tukio hilo kama shambulio la moja kwa moja dhidi ya uhuru wa dini na usalama wa binafsi. Mahmoud al-Khalafi, Mkurugenzi wa Kituo, alisema: “Matukio haya yanakuja wakati ambapo uchochezi na uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu umeongezeka nchini Uswidi, sambamba na hali ya kijamii inayozidi kugawanyika na kubagua.” Polisi wa Sweden wamelichukulia tukio hilo kama uhalifu wa chuki, huku mashirika ya Kiislamu yakitaka ulinzi madhubuti na msimamo wa wazi wa kisiasa.
Uswidi imekuwa uwanja wa matukio ya kuvunjiwa heshima na kudharauliwa kwa Qur’ani Tukufu kwa miaka kadhaa, mara nyingi yakifanyika chini ya kivuli cha sheria za uhuru wa kujieleza.
Rasmus Paludan, mwanasiasa wa mrengo wa kulia, alichoma nakala za Qur’ani Tukufu mara kadhaa, na kusababisha ghasia. Mahakama ya Uswidi ilimhukumu kifungo cha miezi minne kwa uchochezi dhidi ya kundi la kikabila.Salwan Momika, raia wa Iraq aliyeishi Uswidi, alichoma nalaka ya Qur’ani Tukufu nje ya Msikiti wa Stockholm mwaka 2023, na kusababisha hasira katika nchi nyingi za Kiislamu na mvutano wa kidiplomasia. Baadaye aliuawa kwa kupigwa risasi.
Uadui na chuki dhidi ya Uislamu umeongezeka si tu eneo la Scandinavia tu bali pia Ulaya kwa ujumla, sambamba na kupanda kwa vyama vya mrengo wa kulia na sera kali za uhamiaji. Wakati fulani, chuki hizi zilielekezwa kwa Wayahudi; sasa Waislamu wamekuwa mlengwa.
Nchini Marekani, kumekuwa na ongezeko la matukio ya kudharauliwa kwa Qur’ani Tukufu. Mfano ni Jake Lang, mgombea wa Seneti, aliyeshindwa kuchoma nakala ya Qur’ani Tukufu katika maandamano Dearborn, Michigan, baada ya kuingiliwa na Waislamu wa eneo hilo. Baadaye alifanya maandamano Texas, akirekodi video ya kudhalilisha nakala ya Qur’ani Tukufu kwa kutumia kichwa cha nguruwe nje ya msikiti wa Plano.
Mashambulizi haya yanaonyesha kuwa chuki dhidi ya Waislamu imeenea na sasa inahatarisha usalama wa Waislamu popote pale walipo. Qur’ani Tukufu, kitabu kitukufu kinachopendwa na Waislamu, kimekuwa mlengwa wa makundi ya mrengo wa kulia kwa sababu ya nafasi yake ya kiroho. Kama msemo maarufu unavyosema:
3495817