IQNA

Mbunge aliye na chuki dhidi ya Uislamu wa uholanzi awataka Waislamu waritadi

16:56 - May 02, 2012
Habari ID: 2317002
Geert Wilders, mbunge wa Uholanzi aliye na chuki kubwa dhidi ya Uislamu amewataka Waislamu wote duniani waritadi na kutoka kwa umati kwenye duni hii tukufu.
Akizungumza jana Jumanne huko mjini New York Marekani katika sherehe ya uzinduzi wa kitabu chake kipya alichokipa jina la 'Alama ya Mauti: Vita vya Uislamu dhidi Yangu na Magharibi,' mbunge huyo ambaye tayari ametengeneza filamu inayotusi na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu iitwayo Fitna, amesema kwamba amebainisha misimamo yake katika kitabu hicho na kuwataka Waislamu wote ulimwenguni kutoka kwa hiari yao wenyewe katika dini tukufu.
Huku akiendelea kutoa matamshi ya dharau dhidi ya Mtume na Uislamu, mbunge huyo mwenye misimamo ya kupindukia dhidi ya Uislamu amesema iwapo Waislamu watajitenga na Uislamu na kutomkubali Mtume Muhammad kuwa mfano wao wa kuigwa maishani na kutangaza kwamba eti Qur'ani Tukufu ni kitabu kinachochochea utumiaji nguvu, kutatokea mabadiliko makubwa duniani! Wilders amezindua kitabu hicho cha uchochezi dhidi ya Uislamu katika hali ambayo tayari makundi ya kisiasa na shakhsia wa kidini wa Uholanzi wametangaza upinzani wao dhidi ya hatua za chuki za mbunge huyo dhidi ya Uislamu. 998206
captcha