Tovuti ya shorouknews imnukuu Amru al Khidhri ambaye ni mjumbe wa ofisi ya utendaji ya Jumuiya ya Vijana Wanamapinduzi wa Misri akiwataka wananchi wa nchi hiyo kushiriki kwatika maandamano makubwa Ijumaa ijayo kuanzia Msikiti wa Umar Mukarram katika Medani ya Tahrir hadi kwenye ubalozi wa Marekani mjini Cairo kwa shabaha ya kulaani kitendo cha kuchomwa moto nakala za Qur'ani Tukufu katika jimbo la Florida huko Marekani.
Al Khidhri amewataka wanamapinduzi wa Misri wadhihirishe upinzani wao wa kitendo kiovu cha kasisi Terry Jones kwa muchoma moto bendera za Marekani na Israel katika maandamano hayo na kutaka balozi wa Washington afukuzwe nchini Misri.
Amesema kuwa waandamanaji hao watasisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua za kisheria kasisi huyo kwa kosa la kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu kwa mara ya pili na kudumisha uhasama dhidi ya Uislamu.
Amesema kuwa kitendo hicho kiovu cha Kasisi Terry Jones kimedhihirisha mipango ya Marekani ya kuchafua sura ya Uislamu na vita vya nchi hiyo ya kibaguzi dhidi ya dini hiyo. 998616