OIC imesema kitabu hicho ambacho kimeandikwa na Geert Wilders, mbunge wa Uholanzi aliye na chuki kubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu na ambaye tayari ametengeneza filamu inayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu kwa jina la Fitna, kama ilivyokuwa huko nyuma, kimebeba matamshi yasiyo na msingi, ya kichochezi, ya kukaririwa na ya chuki dhidi ya Waislamu.
Imesema mbunge huyo amekuwa akitumia vibaya uhuru wa kujieleza na kifikra, kueneza kampeni ya chuki, hofu na dharau dhidi ya Uislamu.
Huku ikisema kuwa taasisi na vyama vingi vya kisiasa vya Uholanzi vinapinga misimamo ya chuki ya mbunge huyo, OIC imesema kwamba, kitabu hicho kimezinduliwa huko New York Marekani katika hali ambayo Bunge na Umoja wa Ulaya na vilevile serikali ya Uholanzi zimepinga kuzinduliwa kwa kitabu hicho. 999500