IQNA

Timu ya Newcastle kujenga eneo la ibada ya Swala kwa ajili ya wachezaji Waislamu

15:10 - May 07, 2012
Habari ID: 2320513
Kocha mkuu wa timu ya soka ya Newcastle United nchini Uingereza Alan Pardew amesema kuwa klabu hiyo imechukua uamuzi wa kujenga eneo makhsusi kwa ajili ya ibada ya Swala kwa wachezaji nyota Waislamu wa timu hiyo katika uwanja wa nyumbani wa St James’ Park.
Wachezaji Hatem Ben Arfa, Papiss Cisse na Demba Ba ni miongoni mwa nyota wa timu ya Newcastle United msimu huu na kocha wao Alan Pardew ana matumaini kwamba wataisaidia timu hiyo kufanya vyema zaidi.
Kocha Perdew anaamini kuwa itikadi za kidini za wachezaji hao watatu Waislamu zimekuwa na mchango muhimu katika mafanikio ya klabu hiyo katika msimu huu wa ligi ya Premier.
Kocha wa Newcastle ameliambia gazeti la The Mail kwamba amezungumza na mkurugenzi wa klabu hiyo kuhusu suala la ujenzi wa eneo la ibada ya Swala kwa ajili ya wachezaji hao Waislamu kwani viongozi wa klabu wanalazimika kulinda itikadi za kidini za wachezaji wake.
Alan Pardew ameongeza kuwa wachezaji wanapaswa kuheshimiwa na kwamba wachezaji wa ligi kuu ya Uingereza wanafuata dini mbalimbali na kuna udharura wa kujali hali zao. 1001869
captcha