IQNA

'Makumi ya maelfu ya Waitaliano waingia katika dini tukufu ya Kiislamu'

13:59 - May 08, 2012
Habari ID: 2321284
Mkuu wa Muungano wa Taasisi za Kiislamu za Italia (Ucoi) amesema kuwa, hadi kufikia sasa Waitaliano zaidi ya elfu sabini wamesilimu na kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu.
Tovuti ya IINA imemnukuu Elzir Izzedine akisema kuwa, muungano huo hivi sasa unakaribia kukamilisha utafiti wake kuhusu raia wa Italia ambao hadi hivi sasa wameshasilimu na kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu.
Muungano huo wa Taasisi za Kiislamu ya Italia umetabiri kuwa zaidi ya raia elfu sabini wa Italia wamesilimu hadi sasa na kwamba nukta ya kuvutia ni kuwa, idadi ya wanaosilimu inaongezeka siku baada ya siku nchini humo.
Mtandao wa Intaneti wa AGI.it nao umeakisi habari hiyo na kutaja kuwa, moja ya sababu zinazowafanya raia wengi wa Italia waingie katika dini tukufu ya Kiislamu ni hali mbaya sana ya kimaadili na mgogoro mkubwa wa kiuchumi nchini Italia.
Jambo hilo linaonesha kuwa, Waitaliano hivi sasa wamehisi kuwa utatuzi wa mmomonyoko mkubwa wa kimaadili na mgogoro wa kiuchumi unaoikabili nchi yao unapatikana katika dini tukufu ya Kiislamu inayolinda usawa na uadilifu katika kila nukta ya maisha ya mwanadamu.

1003093

captcha