IQNA

Madola makubwa duniani yatumie mantiki katika mazungumzo na Iran'

11:07 - May 12, 2012
Habari ID: 2323207
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amezinasihi nchi za kundi la 5+1 kutumia mantiki kama kigezo katika mazungumzo yajayo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatakayofanyika Mei 23 huko Baghdad, Iraq.
Ayatullah Mohammad Imami Kashani ameongeza kuwa iwapo nchi za Magharibi zinataka kufikia nukta ya pamoja na Iran katika mazungumzo yajayo , zinapaswa pia kuzingatia nafasi muhimu ya Iran katika dunia mbali na kutumia akili na mantiki. Aidha amekumbusha kuhusu fatwa ya iliyotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei kuhusu kuwa haramu utengenezaji silaha za nyuklia. Amesema madola makubwa duniani yanapaswa kuzingtia fatwa hiyo katika mazungumzo ya nyuklia na Iran. Akihutubia waumini katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Kashani amesema nchi za kimagharibi zinapaswa kusitisha sera za uonevu na vitisho dhidi ya Iran. Amesema sasa ni wakati wa Marekani na nchi za Ulaya kuonyesha nia njema kwa kuondoa vikwazo na mashinikizo dhidi ya Iran. Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran pia ametoa salamu za kheri na fanaka kwa munasaba wa kukumbuka kuzaliwa Bibi Fatima Zahra SA, Bintiye Mtume SAW. Amesema Bibi Fatima Zahra SA ni mfano wa kuigwa na wanawake duniani. Ayatullah Kashani amekosoa mtazamo wa wamagharibi kuhusu mwanamke na kusema ukosefu wa misingi imara ya kifamilia katika nchi za Magharibi ni jambo ambalo limewasukuma wanawake Wamagharibi katika ufisadi wa kimaadili.
1005072
captcha