Akizungumza Alkhamisi Mei 11 katika mkoa wa Khorassan Razavi, rais Ahmadinejad amesema hali mbaya ya sasa duniani inatokana na kujiweka mbali na Qur'ani.
Rais Ahmadinejad pia ametahadharisha kuhusiana na matokeo mabaya ya siasa za madola yenye kutaka kujitanua pamoja na ufisadi unaotawala ulimwenguni.
Aidha ameyatahadharisha madola hayo kwamba, muda si mrefu yatakumbwa na takdiri ya Mwenyezi Mungu pamoja na nguvu ya wananchi. Rais Ahmadinejad amesema, madola ya kibeberu ndio chanzo cha matatizo ya jamii ya mwanaadamu. Amesema, madola hayo yamesahau na kuacha njia ya Mwenyezi Mungu na kufuata njia ya shetani. Aidha Dakta Ahmadinejad amebainisha kwamba, daima fikra na vitendo vya madola yanayotaka kujitanua ni ufisadi, dhulma, mauaji, ubaguzi na udhalilishaji.
1004983