Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jumuiya ya Umoja wa Waislamu Ghana imesema mwanasiasa anayegombea kitia cha ubunge William Affum Ani Adjei mashuhuri kama Alajo Obama wa chama cha NDC ameongoza kikao kwa lengo la kupanga njama dhidi ya Waislamu.
Mbunge huyo amedai kuwa kuna mpango wa kuliunganisha bara la Afrika na nchi za Kiarabu na hiyo amewataka Wakristo wachukue hatua za kukabiliana na suala hilo.
Sheikh Annur Sadat mwanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Waislamu Ghana amesema mwanasiasa huyo badala ya kuongoza harakati za amani na maelewano baina ya Waislamu na Wakristo anachochea fitina za kidini na kuivunjia heshima dini ya Kiislamu na Waislamu. Ameitaka serikali ichukue hatia za lazima kukabiliana na matamshi ya mwanasiasa huyo ambayo huenda yakaibua mapigano ya kidini nchini humo.
1007773