IQNA

Vikosi vya Israel vyawajeruhi Wapalestina katika Siku ya Nakba

16:33 - May 17, 2012
Habari ID: 2328006
Zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan baada ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel kuwashambulia Wapalestina waliokuwa wakiandamana katika Siku ya Nakba.
Waandamanaji hao walijeruhiwa huko Qalandiya siku ya Jumanne wakati wakikumbuka tukio la Nakba.
Maandamano makubwa dhidi ya utawala haramu wa Israel yamefanyika katika nchi mbali mbali duniani kwa mnasaba wa kukumbuka tukio la kuanza kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na kuasisiwa utawala bandia wa Israel. Watu wa Palestina wanaitaja siku hiyo kuwa 'Siku ya Nakba' au Siku ya Nakama yaani maafa.
Kati kati ya mwezi Mei mwaka 1948, utawala haramu wa Israel uliundwa baada ya Wazayuni kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
Baada ya kupita zaidi ya miongo sita tokea uundwe utawala wa Kizayuni, bado utawala huo haujaweza kuhalalisha uwepo wake bandia licha ya kutumia kila aina ya ujanja. Maandamano yanayoendelea duniani dhidi ya Wazayuni ni dalili ya wazi kuwa walimwengu hawautambui utawala huo ghasibu.
Kuanzia mwaka 1948 hadi sasa kila mwaka kati kati ya mwezi Mei katika siku ya kukumbuka kuundwa utawala bandia wa Israel, watu wa Palestina na wapenda uhuru kote duniani huandaa maandamano ya kutetea taifa linalodhulumiwa la Palestina.
1009498
captcha