IQNA

Watajiki waanza safari ya kuelekea Hija kwa miguu

17:00 - May 17, 2012
Habari ID: 2328028
Kundi moja la Waislamu kutoka Jamhuri ya Tajikistan wameanza safari ndefu ya kutembea kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Makka kwa lengo la kushiriki katika ibada ya Hija mwaka huu wa 1433 Hijria Qamaria.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA tawi la Kati mwa Asia, kundi hilo ambalo linajumuisha watu wenye umri wa kutoka miaka 21 hadi 65 wameanza safari yao Mei 15 katika mji wa Hamedan mkoani Khatlan nchini Tajikistan.
Amiri wa kundi hilo la mahujaji ni Abdul Aziz Rajabov, mwanaspoti mashuhuri wa Tajikistan ambaye aliwahi kuenda Hija kwa miguu miaka sita iliyopita.
Tajikistan ni nchi ndogo ya Asia ya Kati. Imepakana na Uchina, Afghanistan,Uzbekistan na Kyrgyzstan. Tajikistan haina pwani na bahari yoyote.
Eneo lake ni 143,100 km². Idadi ya wakazi ni milioni 6,5.
Kihistoria maeneo ya Tajikistan yalitawaliwa na madola mbalimbali, hasa na Uajemi.
Uislamu ulifika hapa mnamo mwaka 800 BK.
Mwaka 1868 Tajikistan ilivamiwa na Urusi na kuwa sehemu ya Dola la Urusi na sehemu ya Umoja wa Kisovyet baada ya mapinduzi ya 1917. Iliitwa Jamhuri ya Kisovyet ya Kisoshialist ya Tajikistan.
Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisoviet Tajikistan ilipata uhuru wake mwaka 1991.
Kati ya 1992 hadi 1997 kulikuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyokwisha kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
Uislamu ndio dini rasmi ya Tajikistan. Katika kipindi chote cha utawala wa Kisovieti, watawala wa Kikomunisti walishindwa kuangamiza ustaarabu wa Kiislamu nchini humo.
1008947
captcha