IQNA

Asilimia 66 ya Wapalestina katika Quds kupokonywa makao ya jadi

9:40 - May 22, 2012
Habari ID: 2331200
Mtafiti wa Kipalestina ameficua kuwa zaidi ya asilimia 66 ya Wapalestina waishio Quds watapokonywa makaazi yao ya jadi na Utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na madeni wanayodaiwa na utawala huo ghasibu.
Fakhri Abu Diab amesema utawala haramu wa Israel unatumia sera za kuwarundikia madeni Wapalestina huko Quds na kasha kutumia kisingizio cha madeni hayo kuwatimua katika mji huo. Amesema asilimia kiwango cha umasikini miongoni mwa Wapalestina mjini Quds ni asilimia 78 .
Wakati huo huo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetahadharisha juu ya kuweko mpango wa Wazayuni wa kuiyahudisha Quds yote ifikapo mwaka 2020. Taarifa ya Chama cha Hamas imebainisha kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel umejiandaa kuuyahudisha mji wote mtakatifu wa Quds ifikapo mwaka 2020 na kwamba, njama hiyo imo katika hatua za utekelezwaji.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeashiria pia njama mbalimbali za Wazayuni na kubainisha jinsi nyumba za Wapalestina zinavyobomolewa kila siku sambamba na kasi ya Wazayuni ya kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina. Kadhalika taarifa hiyo ya Hamas imetahadharisha kuhusiana na njama za Wazayuni za kudhibiti vyanzo vyote vya maji katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.
1013376
captcha