IQNA

Upinzani wa moja kwa moja wa Saudi Arabia dhidi ya ushindi wa mgombea wa Ikhwan

18:59 - May 26, 2012
Habari ID: 2334486
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia amemwandikia barua balozi wa nchi hiyo huko Cairo Misri akimfahamisha upinzani wa moja kwa moja wa utawala wa Riyadh dhidi ya ushindi wa Muhammad Morsi mgombea wa chama cha Ikhwanul Muslim katika uchaguzi wa rais wa Misri.
Katika barua hiyo, Waziri Saud al-Faisal wa Saudia amemtaka balozi wa Saudia mjini Cairo kutumia kila njia ili kuhakikisha kuwa mgombea huyo wa Ikhwan anashindwa katika duru ya pili ya uchaguzi huo. Amesema ushindi wa mgombea huyo wa Ikhwan ni hatari kubwa kwa utawala wa Saudia na kwamba utapelekea Saudia kupoteza nafasi yake ya eti uongozi wa ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu! Katika barua hiyo ya siri waziri huyo amemtaka balozi wa Saudia nchini Misri kutumia kila njia ili kudhamini maslahi na siasa za nchi hiyo nchini Misri. Tunakumbusha hapa kwamba kwa mujibu wa matojkeo ya awali ya uchaguzi wa rais wa Misri, Muhammad Morsi mgombea wa Ikhwanul Muslim atachuana katika duru ya pili ya uchaguzi huo na Ahmad Shafiq, Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa dikteta Husni Mubarak. 1017017
captcha