IQNA

Kiongozi wa Kazakhstan akosoa harakati za Mawahabi nchini humo

18:23 - June 10, 2012
Habari ID: 2343721
Pulad Sultanov, mkuu wa taasisi ya uainishaji siasa, inayofungamana na Ofisi ya Rais wa Kazakhstan ametaka kubanwa kwa harakati za Mawahabi nchini humo.
Akiashiria kuenea kwa harakati za kundi hilo psmoja na masalafi nchini Kazakhstan, Sultanov ametaka serikali ichukue hatua za lazima ili kuzuia kuenea kwa harakati za kundi hilo potofu lilanosaidiwa na kudhaminiwa na serikali ya Saudi Arabia. Amesema kuna uwezekano mkubwa wa kutekelezwa vitendo vya ugaidi na makundi hayo katika siku zijazo nchini Kazakhastan kwa lengo la kuvuruga uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hiyo na China. 1026577
captcha