Kwa mujibu wa ripoti hiyo uchunguzi uliofanywa nchini Norway unaonyesha kwamba asilimia 59 ya wananchi wa nchi hiyo wanaamini kwamba utawala haramu wa Israel ni utawala wenye misimamo ya kupindukia mipaka na asilimia 55 inaamini kwamba utawala huo haufuatilii juhudi zozote za kutaka kuwepo amani kati yake na Wapalestina. Asilimia 55 ya Wajerumani pia wanaamini kwamba utawala huo ndio unaochochea ghasia na machafuko katika Mashariki ya Kati, asilimia 46 inaamini kuwa utawala huo umetenda jinai za kibinadamu dhidi ya Wapalestina, asilimia 48 inasema una misimamo ya kupindukia mipaka na asilimia 27 ya wananchi hao wanawaunga mkono Wapalestina. Gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot limemnukuu afisa mmoja wa ngazi za juu katika utawala huo akiwasema kuwa Mayahudi wametengwa sana siku hizi katika nchi za Ulaya kutokana na vitendo vya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina. Amesema utawala huo hivi sasa unafanya juhudi kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ili kurekebisha hali hiyo barani Ulaya. 1026732