IQNA

Maandamano ya kulalamikia uvunjiwaji heshima matukufu ya Kiislamu Tunisia

19:15 - June 16, 2012
Habari ID: 2347947
Baada ya kuandaliwa maonyesho ya sanaa yanayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu nchini Tunisia, wakazi wa mji wa Tatawin nchini humo hapo jana Ijumaa walifanya maandamano makubwa ya kupinga jambo hilo.
Wakazi wa mji huo wamefanya maandamano hayo kulalamikia maonyesho ya sanaa ya hivi karibuni katika mji wa Marsa ulio yapata kilomita 25 kutoka mji wa Algiers.
Waandamanaji wamesema hawakubali hata kidogo kufanyika maonyesho au jambo lolote linalovunjia heshima matukufu ya Kiislamu akiwemo Mtume Mtukufu (saw) na Waislamu. Wamesema Tunisia ni nchi ya Kiislamu na kwa hivyo Waislamu wa nchi hiyo hawataruhusu kuhujumiwa thamani za Kiislamu na baadhi ya makundi ya ndani nchini humo.
Wiki iliyopita miji tofauti ya Tunisia ilishuhudia maandamano ya wananchi wanaopinga na kulalamikia maonyesho hayo yaliyovunjia heshima matukufu ya Kiislamu, jambo lililopelekea kutokea ghasia baina ya waandamanaji na polisi.
Kufuatia malalamiko na maandamano hayo ya Watunisia chama cha Kiislamu cha an-Nahdha kimetaka kubuniwa katika katiba ya nchi hiyo sheria ambayo itaainisha adhabu kwa wale wanavunjia heshima matukufu ya Kiislamu. 1030668
captcha