Katika mahojiano na Televisheni ya Al Alam, Sayyid Nasrallah amesema, 'leo utawala wa Kizayuni wa Israel ni dhaifu kuliko wakati wowote ule.'
Marekani, Israel na waitifaki wao wamekuwa wakitoa vitisho vya kuishambulia Iran kijeshi kwa madai yasiyo na msingi kuwa eti ina mpango wa kutengeneza bomu la atomiki.
Iran imekanusha madai hayo na kusema shughuli zake za nyuklia zinafanyika kwa malengo ya amani na chini ya usimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA na kwa mujibu wa mkataba wa NPT wa kuzuia usambazwaji silaha za nyuklia.
Kinyume na Iran, Israel imekataa kutia saini mkataba wa NPT na inamiliki karibu vichwa 400 vya silaha hatari za nyuklia.
1031672