IQNA

'Hadhi ya Iran imelindwa katika mazungumzo ya nyuklia na kundi la 5+1'

11:57 - June 23, 2012
Habari ID: 2352209
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesema kwamba ujumbe wa Iran katika mazungumzo na kundi la 5+1 umelinda misimamo mitatu ya Jamhuri ya Kiislamu ambayo ni hadhi ya Iran ya Kiislamu, kutumiwa mantiki na ubunifu kivitendo.
Sambamba na kuashiria ukwamishaji wa mazungumo hayo unaofanywa na nchi za Magharibi, Ayatullah Seyyid Ahmad Khatami amesema, kufanyika mijadala tu ya kupoteza wakati hakuna natija yoyote na kwamba iwapo Wamagharibi wanataka kweli mazungumzo hayo yazae matunda, wanapashwa kukiri haki ya taifa la Iran ya kustafidi na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani kwani uzoefu umeonyesha kuwa, kutumiwa vitisho hakutolifanya taifa la Iran lirudi nyuma.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran aidha amekumbusha msimamo wa kimantiki wa Jamhuri ya Kiislamu kuwa matumizi ya teknolojia ya atomiki ni haki ya kila mtu lakini silaha za nyuklia haszipaswi kutumiwa na yeyote, na kusema kuwa Iran mara kadhaa imetangaza kwamba, kamwe haijawahi kuwa na nia ya kutengeneza silaha za nyuklia, uamuzi ambao hautokani na woga bali kwa kuwa ni kinyume na sheria za dini tukufu ya Kiislamu.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran pia amezionya nchi za kundi la 5+1 linalozileta pamoja Marekani, Ufaransa, Uingereza, Uchina, Russia na Ujerumani kutozingatia matamshi ya utawala haramu wa Israel katika mazungumzo ya nyuklia.
1035567
captcha