Washindi walitunukiwa zawadi katika hafla iliyofanyika Ijumaa usiku katika Ukumbi wa Mnara wa Milad mjini Tehran.
Hafla hiyo ilianza kwa kisomo cha Qur’ani cha Qasem Moqaddami na kufuatiwa na hotuba ya Mkuu wa Vyombo vya Mahakama Iran Ayatullah Sadeq Amoli Larijani.
Baada ya hapo Hujjatul Islam Ali Mohammadi mkuu wa Shirika la Awqaf la Iran aliwasilisha ripoti kuhusu mashindano ya mwaka huu.
Katika kitengo cha qiraa Qasem Moghddami kutoka Iran alichukua nafasi ya kwanza , nafasi ya pili ilichukuliwa na Ezzat Al-Seyyed Rashed kutoka Misri huku Mohammad Salman Ali kutoka Bahrain akichukua nafasi ya tatu. Nafasi ya nne ilichukuliwa na Abdulrahman Sabreddin kutoka Indonesia naye Najm Al-Hassan kutoka Bangladesh alishikilia nafasi ya tano.
Katika kitengo cha hifdhi Hussein Mo’tamedi kutoka Iran ameibuka mshindi akifuatiwa na EinulArefin kutoka Bangladesh, Abdollah Omar Hamed kutoka Libya amechukua nafasi ya tatu akifuatiwa na Mahdi Khayrolbalil kutoka Sudan huku Abdulmalek Mohammad Rahim kutoka Afghanistan akichukua nafasi ya tano.
Hafla hiyo ya kufunga mashindano hayo ilihudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwemo Ayatollah Amoli Larijani Mkuu wa Vyombo vya Mahakama Iran, Seyyed Mohammad Hosseini Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran, Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran na Meya wa Tehran Mohammad Baqer Qalibaf.
Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu Iran yalianza Tehran tarehe 27 Rajab ( 17 Juni) kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kubaathiwa Mtume SAW na kuendelea hadi tarehe mbili Shaaban sawa na 22 Juni. Mashindano hayo yalikuwa na washiriki 100 kutoka nchi 65 za Kiislamu za zisizokuwa za Kiislamu.
1035371