Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Jumamosi aliitisha kikao cha dharura cha majenerali wa kijeshi wa utawala huo na kutoa amri ya kushadidishwa mashambulizi dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Amri hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel imekuja huku Wapalestina 17 wakiwemo watoto wadogo watatu wakiwa tayari wameshauawa shahidi na watoto 17 wengine wakiwa wameshajeruhiwa kutokana na mashambulizi mapya ya Israel katika maeneo ya raia huko Ghaza, mashambulizi ambayo yamekuwa yakiendelea kwa wiki nzima sasa. Weledi wa mambo wanasema, ukatili huo mpya wa Wazayuni hauthibitishi kitu kingine ghairi ya kuthibitihsa tabia ya kikatili iliyojengeka katika dhati ya utawala wa Kizayuni. Mashambulizi hayo aidha yanaonesha ni jinsi gani utawala wa Kizayuni wa Israel usivyoheshimu sheria za kimataifa wala misingi ya kibinadamu. Itakumbukwa kuwa, ni utawala huo huo wa Kizayuni ndio uliotaka kufikiwe makubaliano ya kusimamisha vita kati yake na wanamapambano wa Palestina ambapo katika makubaliano hayo, ulikubali kusitisha mashambulizi ya namna yoyote ile katika maeneo ya Wapalestina. Hata hivyo si tu kwamba haikuheshimu makubaliano hayo, lakini pia Israel muda wote imekuwa ikifanya mashambulizi yake dhidi ya wananchi wa Palestina kwa ukatili mkubwa zaidi. Ni jambo linalojulikana wazi kwamba utawala wa Kizayuni hauheshimu kabisa masuala kama amani, mazungumzo, utulivu na usimamishaji vita, bali mara zote umekuwa ukitumia vitu hivyo kama njia tu ya kununua wakati wa kuuwezesha utawala huo kufanya ukatili mkubwa zaidi dhidi ya Wapalestina. Jambo jengine linalowafanya Wazayuni wafanye jinai zao bila ya kujali chochote, ni kimya cha jamii ya kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa. Weledi wa mambo wanasema kuwa, ingawa jinai hizo za Wazayuni zinawaletea matatizo mbalimbali Wapalestina, lakini kamwe haziwezi kuutia doa msimamo makini wa taifa la Palestina wa kusimama imara katika kupigania malengo yake matukufu ya kukomboa kila shibri ya ardhi yake inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
1037575